Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kutoka Tehran, sehemu ya taarifa ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa imesema: Huu ni ushindi na mafanikio makubwa ya kijasusi, sehemu muhimu ya mipango ya busara na hatua za kimya kimya zisizo na kelele za mfumo mtakatifu wa Kiislamu dhidi ya fujo za maadui, ambayo sehemu nyingine muhimu ni juhudi zinazofanywa usiku na mchana na vikosi vya ulinzi katika kuunda uwezo wa operesheni unaolingana na udhaifu na nguvu za utawala wa haramu wa Kizayuni na wanao wakingiabkifua.
Leo hii upatikanaji wa taarifa hizi na kukamilisha mzunguko wa operesheni hii, umewezesha wapiganaji wa Kiislamu kushughulikia mara moja shambulio lolote la utawala wa Kizayuni dhidi ya vituo vya nyuklia vya taifa kwa kushambulia vituo vyake vya nyuklia vilivyo fichwa na kuwapiga hatua kwa hatua dhidi ya vitisho vyovyote vinavyohusiana na miundombinu ya kiuchumi na kijeshi, kulingana na aina ya shambulio.
Maoni yako